IQNA

OIC yalaani hujuma za kigaidi Indonesia, Cameroon

18:49 - January 15, 2016
Habari ID: 3470045
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, OIC, imelaani vikali hujuma za hivi karibuni za kigaidi huko Jakarta mji mkuu wa Indonesia na nchini Cameroon.
OIC yalaani hujuma za kigaidi Indonesia, Cameroon

Katika taarifa, Katibu Mkuu wa OIC Iyyad Amin Madani ameashiria hujuma ya magaidi katika msikiti mmoja huko kaskazini mwa Cameroon ambapo watu 13 waliuawa. Ameituma salamu za rambi rambi kwa serikali ya nchi hiyo na familia za waliopoteza maisha katika hujuma hiyo huku akisisitiza umuhimu wa kupambana na kundi la magaidi wakufurishaji wa Boko Harama katika eneo la Magharibi mwa Afrika.

Itakumbukwa kuwa siku ya Jumatano magaidi walishambulia msikti mmoja katika eneo la Kolofata karibu na mpaka wa Cameroon na Nigeria ambapo watu 13 wameuawa na mwengine mmoja kujeruhiwa.

Kwingineko OIC imelaani hujuma kadhaa za kigaidi Jana Alhamisi katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta. Katibu mkuu wa OIC amesema hakuna chochote kinachoweza kuhalalisha ugaidi huo

Watu wasiopungua saba waliuawa jana na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya milipuko ya mabomu kutokea mjini Jakarta. Eneo lilipotokea hujuma hizo lina shughuli nyingi zikiwemo hoteli za kifahari, balozi na ofisi nyingi za serikali na za binafsi.

Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limetangaza kuhusika na shambulio hilo la kigaidi nchini Indonesia.

3467521

captcha