IQNA

Magaidi Wakufurisahji wa Boko Haram watumia watoto katika ugaidi

14:56 - January 24, 2017
Habari ID: 3470810
IQNA-Magiadi wakufurishaji wa Boko Harm wamekithirisha kutumia watoto wadogo katika harakati zao za kigaidi ikiwemo kutekeleza mashambulizi ya mabomu.
Maafisa wa serikali ya Nigeria wanasema wanachama wanawake wa kundi la magaidi wakufurishaji wa Boko Haram wanawatumia watoto wadogo katika upelelezi wao sambamba na kutekeleza hujuma za kigaidi.
Ripoti hiyo iliyotolewa na maafisa wa serikali ya Nigeria imebainisha kuwa, kutumiwa watoto wadogo katika mashambulizi ya kujitolea muhanga ya kigaidi kumekithiri sana nchini humo, jambo ambalo linawatia wasi wasi mkubwa.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kundi la Boko Haram katika hujuma zake za hivi karibuni limewatumia zaidi, wanawake na watoto wadogo na kwamba mbinu hii imekuwa ikifanikiwa kwa kuwa wanawake na watoto wadodo ni wepesi wa kuepuka vizuizi vya maafisa usalama sambamba na kujipenyeza kwenye mijumuiko na halaiki za watu pasina kushukiwa kuwa wahalifu.

Hii ni katika hali ambayo, Toby Lanzer, Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la magharibi mwa Afrika amesema kuwa, harakati za Boko Haram zimewaweka watoto nusu milioni wa kanda hiyo katika hatari ya kupoteza maisha kutokana na lishe duni. 

Mwezi Aprili mwaka jana, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) lilisema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita Boko Haram wameongeza mara 11 idadi ya watoto wanaotumiwa kufanya hujuma za kigaidi nchini Nigeria na pia katika nchi jirani za Cameroon, Chad na Nigeria.

Neno Boko Haram kwa ya lugha ya Kihausa inayotumiwa na Waislamu wengi Nigeria lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Kundi hilo la Boko Haram ambalo lina ufahamu usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa likitekeleza hujuma katika maeneo mbalimbali ya Nigeria hasa kaskazini mwa nchi hiyo. Tokea kundi hilo lianzishe uasi mwaka 2009 hadi sasa, takribani watu 20,000 wameuawa na wengine takribani milioni mbili wamelazimika kuhama makazi yao.

3462017
captcha