Katika makala aliyoiandikia gazeti la New York Times
Jumatatu, Ban amesema ,"Historia imethibitisha kuwa watu daima watapambana
dhidi ya kukaliw akwa mabavu ardhi zao."
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani pia mpango wa Israel wa kujenga
vitongoji vipya na kunyakua ekari 370 za ardhi za kilimo za Palestina katika
eneo inalolikalia kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi.
Amesema kupuuza dhulma ambazo Israel inawatendea Wapalestina hakuwezi kupelekea
tatizo hilo kutoweka.
Katika siku za hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amebainisha
upinzani wake mkali kuhusu sera za Israel. Mnamo Janauri 26, akihutubu katika
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ban alisema Israel inapaswa kusitisha
ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ili kupigwe hatua kuelekea amani.
Siku iliyofuata, Ban alihutubua katika Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki
za Wapalestina na kusema, Wapalestina, hasa vijana wanapoteza matumaini na wamekasirishwa
na sera za ukandamizaji wa utawala ghasibu wa Israel. Kauli hiyo ilipelekea
waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni kusema kuwa Umoja wa Mataifa unapendelea
upande moja. Katika kujibu matamshi hayo ya Netanyahu, Ban ameandika makala
katika gazeti la New York Times chini ya anuani ya: "Israel, mjumbe
hauawi."
Zaidi ya Waisraeli nusu milioni wanaishi katika vitongoji 230 haramu
vilivyojengwa katika ardhi za Palestina zilizoghusubiwa mwaka 1967 katika
Ukingo wa Magharibi na Quds Mashariki.