Katika hatua isiyo ya kawaida, Baraza la Usalama la UN limepasisha azimio hilo kutokana na muswada uliopendekezwa na nchi nne za Malaysia, Venezuela,Senegal na New Zealand likilaani ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zilizoghusubiwa za Palestina na kutaka ukomeshwe. Azimio hilo limepashwa na nchi 14 wanachama wa Baraza la Usalamamkabala wa kura moja tu ya Marekani ambayo imekataa kulipigia kura.
Kwa mujibu wa azimio hilo, utawala haramu wa Israel unalazimika kusitisha mara moja na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu zaPalestina ikiwemo Quds Mashariki. Vilevile limesisitiza kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi katika ardhi ya Palestina unahatarisha sana mpango wa utatuzi wa mgogoro wa Palestina na ni kizuizi cha kurejeshwa amani.
Kupasishwa azimio hilo ambako hakuna mfano wake katika miaka ya hivi karibuni, kunaweza kutambuliwa kuwa ni matokeo ya mashinikizo ya kimataifa yanayopinga uhalifu unaoendelea kufanywa na Israel huko Palestina na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zilizoporwa na dola haramu la Kizayunimwaka 1967. Vilevile hatua hiyo ni pigo kubwa kwa Israel na waitifaki wake wakuu hususan Marekaniambayo imefanya kila liwezekanalo kuzuia hatua hiyo. Mashinikizo ya kimataifa dhidi ya Israel na washirika wake kwa hakika yalikuwa makubwa kiasi kwamba, hata waitifaki wa Kimagharibi wa Israel kama baadhi ya nchi za Ulaya wamelazimika kupasisha azimio hilo.
Misri ilishawishiwa na Trump kulitupa azimio
Awali azimio la muswada huoliliwasilishwa katika
Baraza la Usalama na Misri. Hata hivyo baadaye serikali ya Misri ilitangaza
kuwa, imeakhirisha zozi la kupigiwa kura muswada huo kutokana mashinikizo
makubwa dhidi yake kutoka Israel na rais mteule wa Marekani Donald Trump ambaye
alimpigia simu Rais Abdul Fattah El Sisi.
Hata hivyo nchi za Malaysia, Venezuela, New Zealand na Senegal jana Ijumaa zilitaka muswada huo unaoilaani Israel upigiwe kuwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Ukweli ni kwamba, msimamo wa Marekani wa kutotumia kura ya veto dhidi ya
muswada huo unaoilaani Israel na kuitaka usitishe mara moja ujenzi wa vitongoji
vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina, umewashangaza wengi. Hii ni
kutokana na ukweli kwamba, katika kipindi cha miaka 8 ya utawala wake, serikali
ya Barack Obama imekuwa ikitumia kura ya veto kupinga na kukwamisha azimio
lolote la kimataifa dhidi ya utawala huo ghasibu. Baadhi ya wachambuzi wa mambo
wanasema, hatua hiyo ya Obama nitangazo la White House la kutoridhishwa
na siasa za Waziri Mkuumwenye misimamo mikali wa Israel, Benjamin
Netanyahu.
Wachambuzi wengine wa mambo wanasema kuwa, msimamo huo wa White House hauna umuhimu mkubwakatika uhusiano wa Washington na Tel Aviv kwa kutilia maanani kwamba,rais mteule wa Marekani, Donald Trump atashika usukani wa nchi hiyo siku chache zijazo. Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Israel amemtuhumu Barack Obama kuwa amechangia katika kupasishwa azimio hilo dhidi ya Israel.
Warepublican wachukizwa na Obama
Vilevile viongozi wa chama cha Republican wameonesha hasira kalidhidi
ya msimamo waWhite House wa kutopiga kura ya veto dhidi ya muswada wa
Baraza la Usalama. Spika wa Kongresi ya Marekani, Paul Ryan amesema, kutopiga
kura ya veto dhidi ya azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama ni aibu kubwa
kwa nchi hiyo. Kabla hapo pia Donald Trump alikuwa ametoa wito wa kupigwa kura
ya veto dhidi ya azimio hilo la Baraza la Usalama. Rais mteule wa Marekani
alisema kuwa, kupasishwa kwa azimio hilo kutaiweka Israel katika nafasi dhaifu
sana katika mazungumzo yake na Wapalestina. Trump anauunga mkono kwa hali na
mali utawala ghasibu wa Israel na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi
katika ardhi za Palestina na hapana shaka kuwa, baada tu ya kushika rasmi
hatamu za uongozi Marekani itapuuza azimio hilo.
Pamoja na
hayo yote inatupasa kusema kuwa, azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa dhidi ya Israel linatoa ujumbe muhimu sana kwa viongozi wa
utawala wa huo wa Kizayuni katika mtazamo wa kisiasa hata kama halina dhamana
ya utekelezaji. Sehemu ya ujumbe huo ni kwamba, kuendelezwa ujenzi wa vitongoji
vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina ni hatua isiyo ya
kibinadamu, ya kidhalimu na kinyume cha sheria kiasi kwamba, hata muitifaki
mkubwa zaidi wa Israel yaani Marekani, ameshindwa kukabiliana na irada na azma
moja ya kimataifa na amelazimika kutotumia kura ya veto na hivyo kutayarisha
uwanja wa kupasishwa kwake.