IQNA

Misri yaandaa mkutano wa kimataifa wa waliohifadhi Qur'ani

16:34 - February 06, 2016
Habari ID: 3470118
Mkutano wa kimataifa wa kutoa mafunzo kwa waliohifadhi Qur'ani unafanyika Misri kuanzia Februari 6-9.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Kongamano hilo limeandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (ISESCO) ambapo waliohifadhi Qur'ani Tukufu (huffadh) kutoka nchi 50 duniani. Huffadh wanaoshiriki katika kongamano hilo linalofanyika mkoani Suez ni wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani ambao wanaendelea na masomo yao katika Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri. Aidha kuna washiriki wanaowakilisha jumuiya na taasisi akdhaa za Qur'ani nchini Misri.

ISESCO imetoa taarifa na kusema kuwa: "Kongamano hili limefanyika kwa lengo la kuimarisha na kustawisha ujuzi wa Huffadh wa Qur'ani sambamba na kuwapa mbinu mpya za kufundisha kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kuwahimiza vijana na watoto kuhifadhi Qur'ani Tukufu."

Taarifa hiyo imesema: "Kongamano hili limeandaliwa kuwasilisha matokeo ya utafiti na uchunguzi katitka uga wa kustawisha taasisi na vituo vya Qur'ani ili kuhudumia kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa njia inayostahiki. Aidha kongamano hili linalenga kuimarisha uhusiano baina ya wataalamu katika uga wa kufundisha kuhifadhi Qur'ani ili waweze kubadilishana uzoefu wao wa kikazi."

3473248

captcha