
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mbali na washiriki Wairaqi, mashindano hayo pia yana washiriki kutoka nchi kadhaa za Kiarabu.
Imearifiwa kuwa mashindano hayo yana washiriki 800 wanaume na wanawake ambapo kutakuwa na vitengo viwili tafauti vya mashindano.
Taasisi ya Kusimamia Haram Takatifu ya Imam Hussein AS imeandaa mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Qarii Seyyed Ali Adel wa Iran alisoma aya za Qur’ani katika sherehe ya ufunguzi mashindano hayo na baada ya hapo kulikuwa na hotuba ya Seyyed Murtadha Jamaluddin, msimamizi wa Darul Qur’ani katika Taasisi ya Kusimamia Haram Takatifu ya Imam Hussein AS. Katika hotuba yake amesisitiza umuhimu wa harakati za Qur’ani katika ili kizazi cha sasa kiweze kufahamu mafundisho ya Qur’ani.
Iraq imeshuhudia ongezeko la harakati za Qur’ani kwa miaka kadhaa sasa tokea kuangushwa utawala wa dikteta Saddam mwaka 2003.