Kikao hicho kilianza kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu ya Qari Ustadh Abbas Salimu na kufuatia na hotuba ya Qarasheikhli ambaye alitoa ripoti fupi kuhusu kongamano hilo.
Katika hotuba yake aliwakumbuka quraa wa Qur'ani Tukufu kutoka Iran ambao waliaga dunia katika maafa ya Mina wakati wa msimu wa Hija nchini Saudi Arabia mwaka jana.
Akihutubu katika kikao hicho, Hujjatul Islam Khamousi alisisitiza ulazima wa kufahamu na kustawisha Qur'ani Tukufu.
Kati ya walioenziwa katika kikao hicho ni wanaharakati wa Qur'ani wakongwe, washindi wa mashindani ya kitaifa na kimataifa ya Qur'ani pamoja na waalimu mashuhuri wa Qur'ani.

