IQNA

17:32 - February 13, 2016
1
Habari ID: 3470134

IQNA, shirika bora zaidi la habari la kitaalamu Iran

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) limechaguliwa kuwa shirika bora zaidi la habari la kitaalamu nchini Iran.

IQNA, shirika bora zaidi la habari la kitaalamu Iran

IQNA imeteuliwa na jobo linalojumuisha wakuu wa mashirika makuu ya habari Iran ambayo imefikia natija hiyo baada ya uchunguzi na tathmini ya miezi kadhaa.

Hii ni mara ya kwanza kurrodheshwa mashirika bora ya habari Iran lengo likiwa ni kuboresha na kuimarisha kiwango cha kazi.

IQNA imepata pointi 73.2 na hivyo kuwa shirika bora zaidi la kitaalamu Iran.

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) ndio la kwanza na la pekee ambalo linashughulikia kwa njia maalumu habari za Quran katika ulimwengu wa Kiislamu. Shirika hili lilianzishwa Novemba 11, 2003 sambamba na tarehe 11 ya Mwezi Aban (Kalenda ya Hijria Shamsia) sawa na tarehe 15 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1424 Hijria Qamaria.

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) hivi sasa linatayarisha habari za Qur'ani kwa lugha 17 hai za dunia zikiwemo: Kifarsi, Kiarabu, Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kiurdu, Kitaliano, Kichina, Kirussia, Kihispania, Kibengali, Kihausa, Kipashtu, Kihindi, Kituruki, Kiazari na Kimalayu.

3475293

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
ANU ABDU
0
0
A/MALEKUM NDUGU WANDISHI OMBI LANGU NKITAKA MNIUNGANISHE HABAR MPATE KWENYE WHATSAP 0773 433268 ZANZIBAR, TANZANIA
captcha