
Wabahrain wameandamana katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo siku ya
Ijumaa ambapo wamelaani jinai za utawala wa Aal Khalifa huku wakitaka
kuachuliwa huru wafungwa wa kisiasa na kupewa haki zao wananchi wa
Bahrain.
Vikosi vya kijeshi Bahrain vimetumia gesi ya simu, mabomu ya sauti na
risasi hai kuwatwanya wananchi waliokuwa wakiandamana kwa amani. Hivi
sasa Bahrain iko katika hali ya hatari wakati wa kukaribia mmaadhimisho
ya Mapinduzi ya wananchi. Ikumbukwe kuwa tokea Februari 14 mwaka 2011,
wakati wa kuanza mapinduzi ya wananchi, takribani kila siku Bahrain
imekuwa medani ya malalamiko na maandamano ya wananchi wanaotaka
mabadiliko ya kisiasa.
Vikosi vya kijeshi vya Saudia na Imarati katika fremu ya 'Vikosi vya
Ngao ya Peninsula' pamoja na askari wa nchi kadhaa za Kiarabu wako
nchini Bahrain kuusaidia utawala dhalimu wa Aal Khalifa kukandamizwa
wananchi. Hatua hiyo ya kukodi wanajeshi wa kigeni imewakasirisha sana
wananchi wa Bahrain na hivyo kuzidisha hasira za wananchi dhdii ya
utawala wa Aal Khalifa.
Matukio ya Bahrain yanaashiria kushika kasi mwamko wa wananchi wa
Bahrain ambao wameazimia kuendeleza harakati za kimapiinduzi. Makundi
ya kimapinduzi Bahrain yametangaza 'uasi wa kiraia' kwa mnasaba wa
kuenzi siku ya kuanza mapinduzi ya wananchi. Mkaundi ya kimapinduzi
Bahrain yamewataka wananchi kufunga maduka yao kuanzia Ijumaa Februari
12 Usiku hadi leo tarehe 14 Februari.
Makundi ya wanamapinduzi Bahrain pia yametaka wananchi wasitishe
ushurukiano wao wa kibiashara na serikali pamoja na benki. Aidha
wananchi wa Bahrain wametakiwa wasiende kazini, shuleni na vyui vikuu
katika siku hizo tatu za uasi wa kiraia. Aidha wamenanchi wa Bahrain
wametakiwa wasitii sheria za kidhalimu na wazuia kuingia mamluko wa
utawala wa Aal Khalifa katika medani za maandamano. Ripoti zinasema
wananchi wa Bahhrain wametii ombi hilo la uasi wa kiraia.
Matukio ya Bahrain ni ishara kuwa wananchi wangali wanaendeleza harakati ya kutetea haki zao.
Takwimu zinaoneysha kuwa maandamano dhidi ya serikali yalishahidi
Bahrain mwaka 2015 na yameimarika zaidi katika mwaka huu wa 2016 na hayo
yote ni ishara ya irada imara ya Wabahrain kufuatilia mwamko wao dhidi
ya utawala wa kiimla wa Aal Khalifa ambao pamoja na kushahididisha
ukandamizaji umeshindwa kuzima irada ya wananchi. Duru za kisiasa
zinadokeza kuwa kushadidi maandamano ya Wabahrain katika wiki za hivi
karibuni ni ishara ya kuimarika mwamako wa Wabahrain na ni pia dalili ya
kufeli fikra za ubanaji na sera za kipolisi za utawala wa Aal Khalifa.
Duru mpya ya mwamko wa wananchi ni ishara kuwa pamoja na kuwepo
ukandamizaji wa Aal Khalifa na tawala zinazounga mkono ukoo huo,
wananchi wangali na uwezo na irada ya kuendeleza mwamko wao hadi pale
yatakapojiri mabadiliko ya kimsingi katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya
Uajemi.
3459350