IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Israel, Saudia zimegonga mwamba katika njama zao Syria

19:04 - February 17, 2016
Habari ID: 3470143
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema njama za Saudia, Israel na Uturuki zimefeli na kugonga mwamba Syria.

Sayyed Hassan Nasrallah aliyasema hayo Jumanne usiku katika hotuba aliyoitoa kupitia televisheni mjini Beirut kwa munasaba wa kuwaenzi wanamapambano waliouawa shahidi wakiwemo Raghib Harb, Abbas Mussawi na Imad Mughniya.

Kiongozi wa Hizbullah amesema: "Maadui wa Syria wamejitayarisha kuanzisha vita latika eneo zima la Mashariki ya Kati na wala hawachukui hatua zozote za kutatua mgogoro wa nchi hiyo kisiasa."

Nasrallah amesema Saudia na Uturuki zimekuwa zikifeli mara kwa mara nchini Syria na ndio sababu zikaanza kutafakari kuhusu kutuma vikosi vya nchi kavu katika nchi hiyo kwa kisingizio cha kupambana na magaidi wa ISIS (Daesh).

Sayyed Nasrallah amesema Israel inahusika katika vita dhidi ya Syria lakini kwamba hadi sasa imeshindwa kwani lengo lake kuu ni kuiangusha serikali ya Syria au kuigawa nchi hiyo vipande vipande.

Ameongeza kuwa Israel inaamini kuwa uwepo wake utakuwa hatarini kutokana na kuendelea kubakia madarakani Rais Bashar al Assad wa Syria.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amebaini kuwa Israel, Saudia na Uturuki zinashirikiana kwa karibu katika njama ya kutaka kumuangusha Rais Assad.

3476296

captcha