IQNA

Shahid Abu Mahdi: Imad Mughniya yungali hai

16:06 - February 14, 2022
Habari ID: 3474928
TEHRAN (IQNA)- Shahidi Abu Mahdi al Muhandis, marhum naibu kamanda wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq, Al Hasdh al Shaabi katika kubainisha sifa za Shahidi Imad Mughniya alisema kuwa yungali hai katika medani za kivita.

Idara ya Habari ya Harakati ya Al Nujabaa nchini Iran, kwa mnasaba wa kukumbuka kuuawa kamanda maarufu Mlebanon, Imad Mughinya ambaye ni maarufu kwa lakabu ya Haj Ridhwan, imesemaba za klipi ya Shahidi Al Muhandis.

Ikumbukwe kuwa, tarehe 12 Februari miaka 14 iliyopita aliuawa shahidi Imad Mughniya maarufu kwa jina la Haj Ridhwan, ambaye alikuwa miongoni mwa makamanda wa Hizbullah ya Lebanon, katika shambulizi la kigaidi lililofanyika mjini Damascus, Syria. Kamanda Mughniya aliuawa katika mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa na vibaraka wa Israel katika gari lake. Shahid Mughniya alijiunga na harakati za mapambano baada ya uvamizi wa Israel nchini Lebanon. Baadaye kidogo alijiunga na harakati ya Hizbullah na kushika nyadhifa za juu katika harakati hiyo. Shahid Mughniya alikuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa Hizbullah dhidi ya Israel katika vita vya siku 33 vya utawala huo nchini Lebanon mwaka 2006.

4036229

captcha