
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tangazo hilo limetolewa na Sheikh Yusuf Adeis, Waziri wa Awqaf na Masuala ya Kidini Palestina ambaye ameongeza kuwa, tayari wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wameanza usajili utakaoendelea hadi Aprili 21.
Ameongeza kuwa mashindano hayo yatakuwa na kategoria tatu za hifdhi, qiraa, na tafsiri.
Mashindano ya Qur'ani ya Al Aqsa yanafanyika chini ya usimamizi wa Wizara ya Awqaf katika maeneo mbali mbali ya Palestina, ameongeza.
Sheikh Adeis amesema washiriki 10 bora katika kila kategoria watapata zawadi. Mashindano hayo yanalenga kusambaza mafundisho matukufu ya Qur'ani katika jamii, amebaini waziri huyo.
Sheikh Adeis ametoa wito kwa Wapalestina kuwasajili watoto wao kushiriki katika mashindano hayo ya Qur'ani.