
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika uamuzi uluotolewa Jumamosi 27 Februari, mahakama ya Misri ilisema Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu inayofungamana na Chuo Kikuu cha Al Azhar inabeba jukumu la kukusanya nakala za Qur'ani zenye makosa ya chapa.
Uamuzi huo umetolewa na Mahakama ya Masuala ya Idara Misri chini ya usimamizi wa Jaji Yahya al Dakruri. Sehemu ya uamuzi huo wa mahakama inasema: "Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Al Azhar na wanaochapisha Qur'ani ndio wanaowajibishwa kuhusu makosa ya chapa katika nakala za Qur'ani. Inaelekea kuwa wahusika hawakuzingait kikamilifu jukumu lao la kulinda amana wakati wa kuchapisha Qur'ani."
Aidha mahakama hiyo imeokosoa Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya Al Azhar kwa kuzembea katika kazi zake kwani taasisi hiyo ina jukumu la kusimamia na inakagua viwanda vya uchapishaji Qur'ani.