
Tawi la Jumuiya ya Jamaat Islami Hind katika wilaya Udupi imeandaa kampeni hiyo ya mwazi moja iliyoanza Ijumaa iliyopita.
Mkuu wa Jumuiya ya Jamaat Islami Hind katika wilayani Udupi ametoa taarifa na kusema lengo la kampeni hiyo, ni kuondoa ujinga na ufahamu potovu kuhusu Uislamu na Waislamu.
Jumuiya hiyo inaamini kuwa kampeni hiyo itaweza kuleta maelewano na kuishi kwa amani watu wote katika jamii.
Katika kampeni hiyo, Jumuiya ya Jamaat Islami Hind itafanya mikutano ya ana kwa ana na watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa kidini, kisiasa na wasomi wa vyuo vikuu. Aidha kamepni hiyo itajumuisha mikutano na wananchi ndani ya kumbi, mashindano ya insha, usambazwaji vitabu na nakala za Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiingereza.