
Sheikh Mohammad Khalil amesema utekelezwaji mpango huo utaanzia katika jimbo la Nabeul na kuenea katika maeneo mengine ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Amesema mkoa wa Nabeul umeteuliwa kuzinduliwa mpango huo kwa sababu ya historia yake ndefu ya harakati za Qur'ani.
Akizungumza akiwa huko Nabeul amebainisha matumaini yake kuwa mpango huo utaweza kuwafunza mahufadh laki moja wa Qur'ani. Aidha akiwa jimboni hapo ametembelea misikiti, vituo vya Qur'ani na jumuiya za Qur'ani.
Amesisitiza kuwa vituo kama hivyo vina nafasi muhimu katika kuwawezesha vijana kuhifadhi Qur'ani. Aidha amesesema wizara yake iko tayari kusaidia vituo hivyo katika kueneza utamaduni wa Qur'ani katika jamii ya Tunisia.