IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani nchini Somalia

20:02 - April 19, 2016
Habari ID: 3470255
Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu nchini yameanza siku ya jumatatu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Ishraq, ambayo inajihusisha na sketa za turathi za utamaduni na elimu.

Mashindano hayo ya siku tano ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu yanawaleta pamoja washiriki kutoka mikoa 18 ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Kati ya walioshiriki katika ufunguzi wa mashindano hayo ni maulamaa wa Kiislamu, na maafisa wa serikali akiwemo Meya wa Mogadishu na Naibu Waziri wa Awqaf na Msuala ya Kiislamu Somalia.

Akihutubu katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo, mkuu wa Jumuiya ya Ishraq Muhammad Abdul Ghani Sidhu ametaja mashindano ya Qur'ani Tukufu kuwa njia muafaka ya kustawisha utamaduni wa Qur'ani katika jamii hasa miongoni mwa vijana.

Wakaazi takribani wote milioni 10 wa Somalia ni Waislamu. Nchi hiyo ya Mashariki mwa Afrika ilitumbukia katika vita vya ndani takribani miaka 25 iliyopita lakini katika miaka ya hivi karibuni usalama umeanza kurejea hatua kwa hatua.

Kishikizo: somalia
captcha