
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sayyid Mustafa Husseini Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Awqaf ametoa tangazo hilo na kuongeza kuwa, vikao hivyo vitahudhuriwa na maqarii sita wa kimataifa kutoka Misri pamoja na maqarii mashuhuri wa kimataifa Wairani.
Sayyid Mustafa Husseini ameongeza kuwa, taasisi za kielimu, kiutamaduni na kisayansi zinahusika katika mahfali na vikao vya kuimarisha ukuruba na mapenzi na Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa mipangilio iliyopo, mwaka huu sawa na miaka iliyopita, katika mahafali hizo za kusoma Qur'ani Tukufu pia kutakuwa na vikao vya qasida.
Mbali na vikao hivyo 400 maalumu vya kusoma Qur'ani, misikiti yote Iran pia huwa na vikao vya Qur'ani hasa baada ya Sala ya Alfajiri na vile vile baada ya sala ya Adhuhuri.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipatia umuhimu mkubwa suala la kuimarisha utamaduni wa Qur'ani kupitia kuandaa programu mbali mbali kama vile maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwaka mjini Tehran katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwka mwezi wa Rajab.
Aidha kitaifa hufanyika harakati mbali mbali zinazohusiana na Qur'ani Tukufu.
3460051