IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Mashariki mwa Afrika yamalizika Djibouti

10:46 - June 23, 2016
Habari ID: 3470412
Mashindano ya 17 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Mashariki mwa Afrika yamemalizika Jumatatu 20 Juni nchini Djibouti.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Duru ya 17 ya Mashindano ya Qur'ani ya eneo la Mashariki mwa Afrika yaliyojumuisha, qiraa, tartil na kuhifadhi Qur'ani Tukufu, mashindano ambayo ni maarufu kama Zawadi ya Rais wa Djibouti, yalianza Alkhamisi tarehe 17 Juni ambapo kulikuwa na washiriki kutoka nchi 10. Mashindano hayo yalimalizika Jumatatu kwa kutangazwa washindi.

Mashindano hayo hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa himaya ya Wizara ya Utamaduni, Awqaf na Masuala ya Kiislamu Djibouti. Kati ya nchi zilizoshiriki katika mashindano ya mwaka huu mbali na mwenyeji Djibouti ni Uganda, Somalia, Sudan, Ethiopia, Kenya, Visiwa vya Comoro na Yemen.

Kwa mujibu wa matokeo ya mashindano hayo wawakilkishi wa Kenya na Sudan ndio waliochukua nafasi za kwanza katika katika kategoria zote tatu za mashindano yaani qiraa, tartil na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Akizungumza katika sherehe za kufunga kikao hicho, Abdul Qadir Muhammad Kamil, Waziri Mkuu wa Djibouti alisema serikali ya Djibouti inaunga mkono harakati za Qur'ani na imefanya kila uwezalo kufanikisha mashindano hayo.

Djibouti ni nchi ndodo ya Mashariki mwa Afrika katika njia ya kistratijia ya baharini ya Babul Mandab na ina ukubwa wa kilomita 400 mraba. Zaidi ya asilimia 95 ya raia wote laki nane wa Djibouti ni Waislamu.

3509524

captcha