Hii ni awamu ya 16 ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani ya Al Aqsa, mashindano ambayo waandalizi wake wanasema yanalenga kuinua kizazi cha waliohifadhi Qur’ani na wenye ujuzi wa Tajwid na ambao pia wanazingatia mafundisho ya Kitabu hicho kitakatifu.
Abdul Hadi Aqa, mkurugenzi wa kitengo cha kuhifadhi Qur’ani katika Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu anasema mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yatakuwa na kategoria nne na yataendelea kwa muda wa siku 12.
Amebaini kuwa kuna washindanon 860 kutoka mikoa mitano ambao wanashiriki katika tukio hilo la Qur’ani katika vitengo vya wanawake na wanaume.
Aqa amesema mashindano hayo yana jopo la majajdi ambao watakuwa na jukumu la kutathmini washiriki na hatimaya kutangaza washindi ambao watapata zawadi ya kuanzia $2000 hadi $4500.
Pamoja na kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unakalia ardhi za Wapalestina sambamba na kuwakandamiza, lakini Wapalestina hawajasita katika kuimarisha shughuli za Qur’ani ikiwa ni pamoja mashindano ya Qur’ani.