Askari huyo anaonekana akitupa kurasa za Qur’ani Tukufu kwenye moto. Vyombo vya habari vya Israel, vikinukuu vyanzo vya kijeshi, vilithibitisha siku ya Alhamisi kwamba mwanajeshi huyo alikuwa amesambaza picha hizo kwenye akaunti yake ya Instagram.
Tukio hili si la kwanza la aina yake. Mwezi Machi, mitandao ya kijamii ilifurika video zikimuonyesha mwanajeshi wa Israel akichana nakala ya Qur’ani Tukufu katika msikiti wa Gaza.
Ripoti zinaonyesha kuwa wanajeshi wa Israel wamehusika katika vitendo vingi vya kuvunjia heshima maeneo matakatifu ya Kiislamu tangu mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba, walipoanza uvamizi wao wa kikatili huko Gaza ambao umeua zaidi ya Wapalestina 35,000 hadi sasa, wengi wakiwa ni wanawake na watoto..
Aidha katika vita vyake, utawala wa Kizayuni wa Israel umebomoa mamia ya misikiti katika Ukanda wa Gaza. Idadi kubwa ya misikiti hii ina umuhimu wa kihistoria na ni miongoni mwa misikiti mikongwe zaidi katika eneo hilo.
3488471