IQNA

Wanawake na Qur'ani

Afisa wa Hamas: Wanawake wa Gaza ni Kama Dhahabu Safi

20:12 - October 30, 2024
Habari ID: 3479673
IQNA - Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, anasema heshima na imani ya wanawake huko Gaza "inang'aa kama dhahabu safi" wakati huu ambapo utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea mauaji ya kimbari na uharibifu katika eneo hilo lililozingirwa.

"Heshima, katika maana zake zote, haiko wazi zaidi kuliko taswira inayoonyeshwa na wanawake wa Gaza," Izzat al-Rishq aliandika kwenye chapisho kwenye akaunti yake ya X, huku akiambatanisha picha ya kundi la wanawake huko Gaza, waliokusanyika kusoma Qur'ani Tukufu katikati ya magofu ya mji wao.
"Hawa wanawake waaminifu wa Kiislamu, ni wamumini ambao wanang'aa kama dhahabu safi katika vita hivi, ni wanawake wenye subira, wahifadhi wa Qur'ani, dada, mama, na wake za wapiganaji na mashahidi," aliandika.
"Wazayuni wasio na heshima wala dhamiri ni kinyume cha kwani wamekuwa wakithubutu kukiuka heshima safi ya wanawake hawa," aliongeza.
Afisa huyo wa Hamas pia aalinukuu aya ya 38 ya Surah al-Hajj, ambayo inasomeka hivi: “Hakika Mwenyezi Mungu atawalinda walio na imani.”
Uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza tangu Oktoba mwaka jana umeua zaidi ya Wapalestina 43,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Takriban Wapalestina wote milioni 2.3 wa Gaza wameyahama makazi yao.

3490478

captcha