IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Maafa ya mina hayatasahaulika

20:14 - September 02, 2016
Habari ID: 3470545
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, watu wa Iran kamwe hawatasahu maafa ya mauti ya kuogofya ya Mina katika msimu wa Hija mwaka jana.

Ayatullah Mohammad Ali Mowahedi Kermani, katika hotuba zake za Sala ya Ijumaa hii leo mjini Tehan ameashiria kuwadia Mwezi wa Dhul Hijja na umuhimu wa Ibada ya Hija na kuongeza kuwa: "Wataalamu wanasema iwapo katika Ibada ya Hija mwaka jana wakuu wa Saudi Arabia wangetekeleza majukumu yao katika kudhamini usalama wa Mahujaji, basi maelfu ya Mahujaji hawangepoteza maisha katika maafa ya Mina."

Ayatullah Mowahedi Kermani amesisitza kuwa, Ibada ya Hija ni adhimu katika Uislamu na kwamba, katika kutekeleza amali za Hija, Waislamu wanapaswa kumfahamu adui na njama zake za kuibua mifarakano.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa pia amebaini kuwa, iwapo Hija itatekelezwa sawa na Hija ya Nabii Ibrahim AS, basi Waislamu hawapaswi kuwa na matatizo. Aidha ameelezea matumaini yake kuwa, Haram Mbili Takatifu ziitakombolewa kutoka mikono ya Mawahabi ili Waislamu waweze kufaidika kikamilifu na Ibada ya Hija sambamba na kutangaza kujibari kwao na maadui wa Uislamu.

yatullah Mowahedi Kermani amewataka watawala wa Saudia kuwa mamluki wa Marekani na hivyo hawaruhusu Waislamu wafaidike ipasavyo na Hija.

3527137

captcha