Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam Seyyed Mustafa Husseini, Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Awqaf na Masuala ya Kiislamu Iran.
Ameongeza kuwa mashindano hayo yatafanyika kuanzaia tarehe 11-17 Mei katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA mjini Tehran.
Kwa mujibu wa Sheikh Mustafa Husseini, mbali na kauli mbiu hiyo kuu kila siku katika mashindano hayo kutakuwa na kauli mbiu maalumu.
Kati ya kauli mbiu hizo ni, "Ummah Moja Waomboleza Maafa" ambapo washiriki watawakumbuka wanaharakati mashuhuri wa Qur'ani waliopoteza maisha katika maafa ya Mina wakati wa msimu wa Hija mwaka jana nchini Saudia. Kauli mbizi zingine ni kuhusu Mtume Muhammad SAW, Mwamko wa Kiislamu na Mapambano (Muqawama) ya Kiislamu.
Sheikh Mustafa Husseini amebainisha kuwa kutakuwa na program zingine pembizoni kama vile maonyesho ya sanaa za Qur'ani n.k.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yamekuwa yakifanyika kila mwaka katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa muda wa miaka 32 sasa.
Mashindano hayo huwaleta pamoja washirki kutoka takribani nchi zote za
Kiislamu na pia nchi zisizo za Kiislamu na washiriki kutoka kila pande ya dunia
hukutanishwa na Qur'ani Tukufu na hivyo kudhihirisha umoja wa Waislamu.