IQNA

Shimon Peres, Muuaji wa Maelfu ya Wapalestina Amekufa

16:18 - September 28, 2016
Habari ID: 3470583
Rais wa zamani wa utawala haramu wa Israel, katili Shimon Peres ameaga amekufa usiku wa kuamkia leo, wiki mbili baada ya kupatwa na kiharusi

Duru za Kizayuni zkimetangaza kuwa Peres alikufa saa tisa na dakika 40 usiku wa kuamkia leo kwa wakati wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu baada ya kukimbizwa hospitalini hapo kutokana na matatizo ya kiafya. Hali ya mtawala huyo katili wa zamani wa Israel ilitangawa kuwa mbaya na kuingizwa moja kwa moja katika kitengo cha wagonjwa mahututi. 

Katika uhai wake wa kisiasa ulioendelea kwa kipindi cha miongo saba  Peres alishika nyadhifa mbalimbali katika utawala haramu wa Israel. Aliwahi kuwa Rais wa Israel, Waziri Mkuu na Mkuu wa Majeshi ya utawala huo ghasibu. 

Katika kipindi cha uongozi wa Shimon Peres, Wapalestina wasiopungua elfu nne waliuawa katika vita mbili tofauti zilizoanzishwa na utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza kati ya mwaka 2007 na 2014. 

Katika vita ya pili iliyoanza July 8, 2014 na kumalizika  August 26, Wapalestina 11,100 wakiwemo watoto 3,374 na wanawake 2,088 pia walijeruhiwa.

3461040

captcha