Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mtaalamu mmoja wa Uingereza, Marc Owen Jones amesema amefanya utafiti na kugundua maelefu ya akaunti bandia katika mtandao wa kijamii wa Twitter ambazo zina hashtag zenye kueneza fitina na chuki dhidi ya Ushia, Mashia na Iran.
Mtaalamu huyo wa Uingereza amesema baada ya utafiti wa muda mrefu, amebaini kuwa baadhi ya akaunzi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuongoza magaidi wa ISIS na kuhimiza kuwataja Mashia kuwa ni Rafidha.
Ameongeza kuwa akaunti hizo hufanya kazi katika muda maalumu wa siku na kutuma maelfu ya jumbe kwa muda wa saa moja. Jones anasema kuwa, idadi kubwa ya akaunti hizo inaelekea kuwa ni za Saudi Arabia yaani takribani akaunti milioni moja ambazo ni asilimia 40 ya akaunti zote za Twitter Mashariki ya Kati (Magharibi mwa Asia). Mtaalamu huyo wa Uingereza amesema kwa siku, takribani jumbe 10,000 kutoka akaunti hizo zinatiliwa shaka kwani hutoka sehemu moja na aghalabu zinahusu sera kigeni za Saudi Arabia.
Inafaa kuashiria hapa kuwa bilionie Msaudi, Mwanamfalame Al-Waleed Bin Talal bin Abdulaziz al Saud anamiliki hisa milioni 35 katika hirika la Twitter na hivyo kumfanya kuwa wa pili kwa idadi kubwa ya hisa katika mtandao huo wa kijamii.