TEHRAN (IQNA)-Maimamu wa Kishia ni kumi na wawili kutoka katika kizazi cha Mtume Muhammad SAW ambao kwa mujibu wa riwaya za kuaminika, ni warithi wa Mtume na baada yake wanatambulika kama Maimamu wa jamii ya Kiislamu. Mashia wanaamini kwamba Maimamu hawa wamechaguliwa na Mungu, lakini kwanini?
Habari ID: 3475037 Tarehe ya kuchapishwa : 2022/03/14
IQNA-Serikali ya Uturuki imelaaniwa vikali kwa kuamuru kufungwa televisheni mbili za Waislamu wa madhehebu ya Shia ambazo zilidaiwa kueneza "propaganda dhidi ya serikali".
Habari ID: 3470811 Tarehe ya kuchapishwa : 2017/01/25
IQNA-Saudi Arabia inaendeleza vita vya siri dhidi yay a Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na, Ushia na Waislamu wa madhehebu ya Shia kupitia akaunti bandia za mitandao ya kijamii, imefichuliwa.
Habari ID: 3470656 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/11/06
Mwanafunzi wa zamani wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, amebainisha wasiwasi wake kuhusu hali ya kiafya ya mwanazuoni huyo.
Habari ID: 3470243 Tarehe ya kuchapishwa : 2016/04/12
Kiongozi mwandamizi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Uganda Sheikh Ductoor Abdul Qadir Sudi Muwaya aliuawa shahidi Alkhamisi iliyopita. Mkuu wa polisi nchini humo ametangaza kuwa uchunguzi wa kina utafanyika kubainisha aliyetekeleza mauaji hayo.
Habari ID: 2646978 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/29
Kongamano la Kimataifa la ‘Hatari ya Misimamo Mikali Na Utakfiri Kwa Mtazamo wa Maulamaa wa Kiislamu’ lilianza jana hapa nchini Iran katika mji Mtakatifu wa Qum kusini mwa Tehran kwa kuhuduriwa na mamia ya maulamaa na wanafikra wa Kiislamu kutoka madhehebu ya Shia na Sunni.
Habari ID: 2611223 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/24
Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemwandikia barua Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudi Arabia ya kumtaka azuie kutekelezwa hukumu ya adhabu ya kifo iliyotolewa dhidi ya mwanazuoni wa Kishia wa nchi hiyo Sheikh Nimr Baqir an-Nimr.
Habari ID: 1463760 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/10/26
Muungano wa Wasomaji Qurani Tukufu nchini Misri umemfutia uanachama wa muungano huo Sheikh Farajullah al Shadhilii mmoja kati ya wasomaji Qurani Tukufu mashuhuri nchini Misri kwa sababu tu ya kuadhini kwenye Msikiti wa Kishia nchini Iraq.
Habari ID: 1407016 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/05/15