IQNA

Nigeria yatakiwa na ICC kutoa maelezo kuhusu mauaji ya Waislamu

6:29 - November 18, 2016
Habari ID: 3470683
Hatimaye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imeitaka serikali ya Nigeria kutoa maelezo kuhusu mauaji yaliyofanywa mwaka jana na jeshi la nchi hiyo dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji wa Zaria.

IQNA-Hatimaye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imeitaka serikali ya Nigeria kutoa maelezo kuhusu mauaji yaliyofanywa mwaka jana na jeshi la nchi hiyo dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji wa Zaria.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Trust kuwa, baada ya wito huo wa ICC, Waziri wa Sheria wa Nigeria ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo, Abubakar Malami ameelekea The Hagua nchini Uholanzi kwa ajili ya kueleza nafasi ya jeshi la nchi yake katika mauaji hayo.

Ikumbukwe kuwa kati ya Disemba mwaka 2015, Jeshi la Nigeria liliwashambulia wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeriakatika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Jeshi hilo lilidai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Allamah Sheikh Ibrahim Zakzaky walikuwa na njama ya kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo. Jeshi hilo katili liliizika miili ya waliouawa katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo. Inakadiriwa kuwa Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa katika tukio hilo huku Sheikh Zakzaky, ambaye hali yake ni mahututi, akiendelea kushikiliwa korokoroni pasina kufunguliwa mashtaka.

Jumatatu wiki hii pia Waislamu wasiopungua 100 wa madhehebu ya Shia waliuawa nchini Nigeria kwa kupigwa risasi na jeshi la nchi hiyo.

Waislamu hao waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa walipokuwa katika mjumuiko huo wa kidini nje kidogo ya mji wa Kano ulioko kaskazini mwa Nigeria.

Wachambuzi wa mambo wanadokeza kuwa wanasema Jeshi la Nigeria linawashambulia na kuwaua kiholela Waislamu wa madhehebu ya Shia katika fremu ya kutekeleza sera za utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia.

3546688

captcha