IQNA

Kijiji cha Iran chenye idadi kubwa zaidi ya watu waliohifadhi Qurani duniani

11:26 - January 21, 2017
Habari ID: 3470806
IQNA: Quranabad ni kijiji kilicho katika mji wa kusini mwa Iran wa Shiraz ambapo wanakijiji waka 63 wamehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.
Kijiji cha Iran chenye idadi kubwa zaidi ya watu waliohifadhi Qurani duniani

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kijiji hicho chenye idadi ya watu 1200, kimetajwa kuwa kilicho na idadi kubwa zaidi ya waliohifadhi Qur'ani duniani kwa kuzingatia ukubwa na idadi ya watu.

Mwaka 1996 kulianzishwa jitihada za kukifanya kijiji hicho, wakati huo kikujulikana kama Mohammadabad, kuwa kijiji cha Qur'ani.

Wakati huo kulikuwa hakuna mtu yeyote aliyekuwa amehidafhi Qur'ani kikamilifu kijijini Mohammadabad na kwa msingi huo wahubiri wa Kiislamu waliofika hapo walianza mkakati maalumu wa kustawisha utamaduni wa kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Wahubiri hao walizindua taasisi ya kiutamaduni ya Qur'ani iliyojulikana kama Bayt al-Ahzan Hadhrat Zahra (SA) ambayo ilianza kuandaa vikao maalumu vya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Baada ya muda usio mrefu taasisi hiyo ilieneza wigo wake kitaifa ambapo sasa ina matawi 165 kote Iran.

Mwaka 2001 kulizinduliwa shule maalumu ya kuhifadhi Qur'ani kijijini Mohammadabad na baada ya mwaka moja wanafunzi wake saba waliweza kuhifadhi Qur'ani kikamilifu.

Baada ya muda, si tu kuwa wanakijiji wa Mohammadabad walikuwa wakisoma na kuhifadhi Qur'ani katika madrassah hiyo bali pia wakaazi wa vijiji na miji ya karibu na hata raia wa nchi kama vile Afghanistan na Indonesia walijisajili kusoma hapo.

Hadi sasa wanafunzi 200 waliohifadhi Qur'ani kikamilifu wamehitimu kutoka chuo hicho, wakiwemo wakaazi 63 kutoka kijiji cha Mohammadabad ambacho sasa kinajulikana kama Qur'anabad. (kiambishi tamati cha 'abad' kwa lugha ya Kifarsi kina maana ya kijiji; hivyo Quranabad ina maana ya kijiji cha Qur'ani)

http://iqna.ir/en/news/3461950


Kijiji cha Iran chenye idadi kubwa zaidi ya watu waliohifadhi Qurani duniani

captcha