IQNA

Kiongozi Muadhamu apongeza jitihada za wazima moto katika maafa ya jengo la Plasco mjini Tehran

14:56 - January 30, 2017
Habari ID: 3470822
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amepongeza kujitolea kwa wahudumu waumini na mashujaa wa kikosi cha zimamoto katika tukio la kuungua na kuporomoka jengo la kibiashara la Plasco jijini Tehran.
Katika ujumbe aliotuma Jumapili usiku, Ayatullah Sayyed Ali Khamenei alisisitiza kwamba, wananchi wote wa Iran wanapaswa kujifakharisha na azma na ushujaa ambao chimbuko lake ni imani.

Kiongozi Muadhamu amesema katika ujumbe wake huo kwamba, kujitolea huku kwa wahudumu wa kikosi cha zimamoto kwa ajili ya kuokoa roho na mali za wananchi wenzao kuliwafanya wahudumu hao wakiwa na ushujaa wa kushangaza kuingia ndani ya moto na kuhatarisha maishana roho zao.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mashahidi hawa kwa mara nyinhgine tena wamehuisha kumbukumbu za kujitolea katika kipindi cha kujihami kutakatifu wakati wa vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na utawala wa dikteta Saddam Hussein dhidi tya Iran.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, mashahidi wa kikosi cha zimamoto wameonyersha kwamba, Muirani muumini akiwa na azma na ushujaa ni mfano wa kuigwa katika njia ya Mwenyezi Mungu na yuko tayari kujitolea maisha yake bila kusita.

Jengo la kibiashara la Plasco mjni Tehran liliungua moto na kisha kuporomoka Alkhamisi ya tarehe 19 Januari. Wafanyakazi 16 wa kikosi cha zimamoto waliokwenda kuokoa watu na kufanya juhudi za kuuzima moto huo walipoteza maisha yao na wananchi wengine wanne baada ya kuangukiwa na jengo hilo na kufukiwa na kifusi. Shughuli ya mazishi ya mashahidi wa kikosi cha zima moto imefanyika leo katika Makaburi ya Behesht Zahra SA kusini mwa Tehran.

3462209


captcha