Akiwasilisha makala yenye anuani ya "Mimea ya Kitiba Katika Qur'ani" katika Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Taaluma Kadhaa za Masomo ya Qur'ani ambalo limefanyika Tehran, Dkt. Abdulmalik Ahmed Idris amesema, kwa kufanya utafiti kuhusu aya za Qur'ani ambazo masuala ya kitiba yametajwa, Waislamu kwa mara nyingine wanaweza kuiongoza dunia katika sekta ya dawa na tiba.
Msomi huyo wa Chuo Kikuu cha Gadarif cha Sudan amesema mimea iliyotajwa katika Qur'ani ina faida nyingi sana za kitiba na kinyume cha dawa ya kemikali haina madhara.
Akiashiria utafiti wake amesema, matokeo ya ya uchunguzi wake yamebaini kuwa mimea iliyotajwa katika Qur'ani ina faida nyingi za kitiba ambazo zimegunduliwa katika miongo ya karibuni.
Kongamano la Kwanza Kimataifa la Taaluma Kadhaa za Masomo ya Qur'ani lilianza Jumatatu katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo makala 39 zinawasilishwa katika mkutano huo wa siku tatu wa wasomi wa kimataifa.