IQNA

Wanawake Waislamu London wafungamana na waathirika wa ugaidi

10:38 - March 28, 2017
Habari ID: 3470911
TEHRAN (IQNA)-Wanawake Waislamu mjini London wamekusanyika katika Daraja la Westminster na kuunda mnyororo wa binadamu (human chain) kubainisha kufungamana kwao na waathirika wa hujuma ya kigaidi wiki iliyopita katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mjumuiko huo wa Jumapili uliwaleta pamoja wanawake karibu 100 ambao walishikana mikoni huku wakiwa wamenyamaza kimya kama njia mojawapo ya kulaani ugaidi huo na kubainisha kufungamana kwao na waathirika.

Jumatano iliyopita, gaidi aliyetmabulika kama Khalid Masood aliendesha gari katika njia ya miguu karibu na bunge la Uingereza na kuwaua wapita njia watatu kabla ya kumdunga kisu afisa wa polisi. Gaidi huyo naye pia alipigwa risasi na kuuawa.

Daktari Sarah Wassem amesema ameshiriki katika mjumuiko huo ili kuonyesha kuwa wanawake Waislamu wanajali yanayojiri duniani. Wanawake hao Waislamu wamekusanyika hapo baada ya makundi ya wazungu wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia kuanzisha kampeni dhidi ya wanawake wanaovaa Hijabu baada ya hujuma hiyo ya London.

Kwigineko, imebainika kuwa gaidi aliyetekeleza hujuma hiyo aliwahi kuwa mwalimu wa Kiingereza nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza, Khalid Masood alifungwa jela mara ya kwanza mwaka 1983 akiwa na umri wa miaka 19 na aliwahi kupatikana na hatia ya vitendo kadhaa vya jinai hadi mwaka 2003. Baada ya hapo alipata cheti cha TESOL cha kufunza lugha ya Kiingereza kwa wazugumzaji wa lugha nyinginezo.

Cheti hicho kilimuwezesha kupata kaziya kufunza Kiingerezanchini Saudi Arabia katika mji wa Yanbu mwaka 2005. Baada ya hapo alijiunga na Shirika la Usafiri wa Anga Saudi Arabia (GACA) mjini Jeddah. Alirejea Uingereza mwaka 2009 na kuendelea na kazi ya kufunza lugha ya Kiingereza.

Shirika la Usalama wa Ndani Uingereza MI5 linasema Masood aliwahi kuchunguzwa kutokana na misimamo mikali ya kufurutu ada na tabia za utumiaji mabavu. Masood aliyekua na umri wa miaka 52 alijulikana kwa majina ya Adrian Elms na Adrian Ajao kabla ya kusilimu. Kundi la kigaidi la ISIS lilidai kuwa shambulio hilo limefanywa na mfuasi wake.

3585823

captcha