Profesa Rodney Shakespeare ameyasema hayo alipokuwa katika mjadala wa televisheni kuhusu uchunguzi mpya wa maoni unaoonyesha kuwa Waingereza waliowengi wanapinga hatua ya nchi yao kuiuzia Saudi Arabia silaha.
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na Opinium kwa niaba ya Kampeni Dhidi ya Biashara ya Silaha (CAAT) umeonyesha kuwa karibu asilimia 62 ya raia wote wa Uingereza wanaamini kuwa kuuziwa Saudia silaha ni jambo lisilokubalika. Saudia ndie mnunuzi mkubwa zaidi wa silaha za Uingereza.
Serikali ya Uingereza imekuwa chini ya mashinikizo ya makundi ya haki za binadamu kusitisha uuzaji wake wa silaha kwa Saudia. Tokea Machi 2015 wakati Saudia ilipoanzisha hujuma haramu dhidi ya Yemen, Uingereza imeuuzia utawala huo wa Riyadh silaha zilizogharimu Pauni Bilioni 3.3. Hadi sasa vita hivyo vimeua zaidi ya Wayemen 11,400 wengi wakiwa ni raia wa kawaida hasa wanawake na watoto.
Katika mahojiano na Press TV, Shakespeare amesema. "Kuna njama kubwa katika kuuziwa Saudia silaha za Uingereza."
"Uingereza inauunga mkono utawala wa Saudi Arabia kama sehemu ya kuandaa vita vikubwa vinavyokuja Mashariki ya Kati, ambavyo ni kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel," ameongeza.
Msomi huyo mtajika amebaini kuwa, Wazayuni katika serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May wanataka kuanzisha vita dhidi ya China, Russia na mataifa ya Mashariki ya Kati (Asia Magharibi).
Akiashiria hatua ya hivi karibuni ya Trump kuwapiga marufuku raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia Marekani, Profesa Shakespeare amesema hatua hiyo ni sehemu ya kuandaa mazingira ya vita vikubwa dhidi ya Uislamu.
"Siasa za Uingereza zinongozwa na Uzayuni na nchini Marekani Trump ameteua Mzayuni baada ya Mzayuni na hii ndio sababu ya Saudi Arabia na Qatar kutowekwa katika orodha ya nchi ambazo raia wake wamepigwa marufuku kuingia Marekani," amesema. Aidha Profesa Shakespear ameitaja Saudi Arabia kuwa ni mwanzislishi wa pote la Uwahhabi na kusema utawala wa Riyadh unaendelea kuunga mkono pote hilo kifikra na kifedha.
Msomi huyo wa Uingereza ameendelea kubaini kuwa, "kile kinachojiri sasa si uuzaji wa silaha tu, bali ni mpango wa kuhakikisha kuwa Uzayuni utaenea katika nchi zote za Mashariki ya Kati na kimsingi hazitakuwa nchi huru tena." Amesema ni Jamhuri ya Kiislamu tu itakayobakia kuwa nchi yenye uhuru halisi na yenye kujitegemea Mashariki ya Kati.