Kufautia malalamiko ya wazazi na wanaharakati waliosema vitambulisho hivyo ni vya kibaguzi, Shule ya Upili ya Northcliff mjini Johannesburg wiki hii imelazimika kuondoa kitambulisho hicho.
Waziri wa Elimu wa Mkoa wa Gauteng, Panyaza Lesufi amesema amezungumza na mkuu wa chuo hicho ambaye ameafiki kubatilisha kadi au kitambulisho hicho maalumu.
Mwanaharakati wa kijamii
Yusuf Abramjee amesema aliwasilisha malalamiko kwa waziri huyo kufuatia
malalamiko ya wazazi. Naye Abeedah Adams, mzazi katika shule hiyo amesema
bintiye alilazimika kubeba kitambulisho hicho kila wakati alipokuwa shuleni ili kuruhusiwa kuvaa
hijabu. Amelinganisha kitendo hicho na sera za mfumo wa ubaguzi wa rangi
uliokuwepo Afrika Kusini ambapo wazalendo weusi walilazimishwa kubebe
vitambulisho maalumu kusafiri kutoka mji moja hadi mwingine. Abramjee amesema wazazi wamempongeza waziri
wa elimu kwa kuchukua hatua za haraka kuhusu suala hilo.
Katiba ya Afrika Kusini inaruhusu uhuru wa kuabudu na inapinga ubaguzi wowote kwa msingi wa kidini.
Waislamu ni zaidi ya asilimia mbili ya watu wote milioni 50 Afrika Kusini na wanashiriki katika sekta zote za kiuchumi nchini humo.