Katika kuchunguza kadhia hiyo, Televisheni ya ITV
iliwatuma wanawake watatu kikachero ambao walijiunga na makundi ya mrengo wa
kulia yenye misimamo mikali likiwemo kundi linalopinga wahamiaji la Generation
Identity.
Kundi hilo linalenga kuleta pamoja harakati za kitaifa za vijana Wazungu Ulaya ili kulina kile wanachosema ni kuhatarishwa utambulisho na utamaduni wa Wazungu barani Ulaya kufuatia ongezeko la wahamiaji na kuenea Uislamu barani huo.
ITV imeerusha hewani filamu inayowaonyesha vijana hao wenye misimamo mikali wakiwa Ufaransa kupata mafundisho yanayoshabihiana na ya kijeshi katika kambi za kundi la Generation Identity.
Kuongezeka wimbi la vyombo vya habari vinavyoeneza chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya kumewaweka katika wakati mgumu sana Waislamu barani humo kiasi kwamba uchunguzi wa hivi karibuni wa maoni unaonesha kuwa, kati ya kila watu watano wa barani Ulaya, mmoja anachukia kuwa na jirani Muislamu.
Zenye maoni mengi zaidi