IQNA

11:15 - December 01, 2017
News ID: 3471289
TEHRAN (IQNA)-Idadi ya Waislamu barani Ulaya imekadiriwa kuongezeka kutoka milioni 25 hivi sasa hadi kufikika milioni 76 ifikapo mwaka 2050, uchunguzi umebaini.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Shirika la Utafiti la Pew chini ya anuani ya , "Ongezeko la Idadi ya Waislamu Barani Ulaya”, kuongezeka Waislamu Ulaya kutategemea wahajiri wanaoelekea katika bara hilo kutoka nchi zenye Waislamu wengi.

Uchunguzi huo umebaini kuwa iwapo mkondo wa sasa wa wimbi la wahajiri Waislamu litasitishwa kikamilifu, idadi ya Waislamu Ualya itaongezeka kutoka asilimia 4.9 ya sasa hadi asilimia 7.4 au takribani milioni 36 ifikapo mwaka 2050.

Katika mtazamo wa pili iwapo kutakuwa na kiwango cha wastani cha wahajiri wa kawaida pasina kuwepo wakimbizi wanaokimbia vita au ukosefu wa uthabiti katika nchi zao basi idadi ya Waislamu barani Ulaya itakuwa ni asilimia 11.2 au milioni 59 ifikapo mwaka 2050.

Katika mtazamo wa tatu, iwapo hali ya hivi sasa ya wimbi la wakimbizi wanaomiminika barani Ulaya litaendelea kama ilivyokuwa baina yam waka 2014 na 206, basi Waislamu watakuwa asilimia ya watu wote barani Ualya au takribani milioni 75 hii ikiwa ni karibu ongezeko la mara tatu la idadi ya sasa.

Katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la wakimbizi wanaoingia Ulaya kutoka nchi zenye Waislamu wengi. Idadi kubwa ya wakimbizi hao wameingia Ujerumani, Italia na Ugiriki.

Mbali na kuongezeko idadi ya Waislamu Ulaya kutokana na wimbi la wahajiri hivi sasa pia kunashuhudiwa idadi kubwa ya wenyeji asili wa Ulaya wakisilimu na kufuatia Uislamu maishani.

3464568

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: