IQNA

11:12 - December 18, 2017
News ID: 3471315
TEHRAN (IQNA) Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu Nigeria amekosoa namna wanawake Waislamu wanaovaa Hijabu nchini humo wanavyosumbuliwa.

 

 

Bi. Amasa Firdaus Abdulsalam

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake katika Kongamano la Kitaifa la Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu Nigeria, Alhaji Muhammad Sa’ad Abubakar III alisema Waislamu wanapaswa kupewa ruhusa ya kutekeelza misingi yao ya kidini kwa mujibu wa maamurisho ya Mwenyezi Mungu SWT na Sunna ya Mtume SAW.

Alhaji Abubakr ambaye pia ni Sultan wa Sokoto (Eneo la Waislamu Kaskazini mwa Nigeria) aliongeza kuwa, uhuru wa kuabudu uko wazi katika katiba ya NIgeria na hivyo ni jambo linaloshangaza kuona Waislamu nchini humo wananyimwa haki zao na kubughudhiwa kwa sababu tu wanazingatia vazi la Hijabu. Kauli hiyo imekuja baada ya wakili moja Muislamu kunyimwa leseni ya kufika mahakamani kwa sababu ya kuvaa Hijabu. Alhaji Abubakr amekosoa Baraza la Masomo ya Sheria Nigeria kwa kukataa kumpa leseni Bi. Amasa Firdaus Abdulsalam  ambaye amehitimu katika taalmu ya sheria kutoka katika Chuo Kikuu cha Ilorin.

Bi. Amasa alikataa agizo la kuvua Hijabu yake katika sherehe za kuwakabidhi leseni mawakili wapy waliohitimu katika taaluma hiyo wiki iliyopita.

Katika hotuba yake iliyosomwa Jumamosi na Profesa Sanni Abubakr Lugga alisema, "Hijabu si vazi la Kiislamu tu bali pia Wakristo na kila mwanamke mwenye kujiheshimu huvaa vazi hilo. Ni vazi la kila mwanamke anayetaka kujisitiri hadharani."

Ameshangaa ni kwa nini Bi. Amasa amezuiwa kuvaa Hijabu wakati jaji mkuu wa zamani wa Nigeria Zainab Bulkachuwa alikuwa akivaa Hijabu na pia majaji wengine nchini humo wamekuwa wakivaa hijabu bila tatizo lolote.

Kesi hiyo imepeleka kuibuka kampeni kubwa katika mitandao ya kijamii chini ya anuani ya #JusticeforFirdaus 

3673448

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: