Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA awamu ya mchujo wa mashindano hayo itafanyika katika Kituo cha Kiislamu cha SABA ambapo wale watakaofika fainali watashindano katika Kituo cha Kiislamu cha Fatimya California Kaskazini. Mashindano hayo yanatazamiwa kufanyika baina ya Mei 5 hadi Mei 12.
Kituo cha Kiislamu cha SABA, katika mji wa San Jose, jimboni Califronia na kilifunguliwa katika muongo wa 80. Kituo hicho kuwa na harakati kadhaa za Kiislamu na kimeweza kufaunikiwa kuhudumia jamii ya Waislamu katika eneo hilo la Marekani.