IQNA

22:27 - May 21, 2018
News ID: 3471525
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Uturuki yameanza Jumapili mjini Istanbul.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yanafanyika katika Msikiti wa Fateh mjini humo na washiriki wanachuana katika kategoria mbili za qiraa au kusoma na kuhifadhi Qur’ani kikamilifu.

Mashindano ya qiraa yanafanyika kila sikua kuanzia saa sita hadi saa tisa mchana na kategoria ya kuhifadhi inaanza saa tano usiku hadi saa saba usiku.

Kuna washiriki 50 katika kategoria ya qiraa na 60 katika kategoria ya hifdhi kutoka juma ya nchi 60 ambao watashindani hadi fainali iliyopangwa kufanyika Mei 30.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawakilishwa na Mohammad Reza Ahmadi katika kategoria ya hifdhi huku  Omid Hosseininejad akishiriki katika qiraa.

/3716331

 

 

 
 
Name:
Email:
* Comment: