IQNA

Harakati za Qur'ani

Qari wa Iran alinganisha Iran na Uturuki katka Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani

20:31 - November 02, 2024
Habari ID: 3479688
IQNA - Seyed Parsa Angoshtan, qari wa Iran aliyeshika nafasi ya pili katika mashindano ya 9 ya kimataifa ya Qur'ani Uturuki mapema wiki hii amezungumza kuhusu hayo nay ale yanayofanyika nchini Iran.

Akizungumza na IQNA baada ya kurejea nyumbani, Angoshtan alisema kuna  tofauti kubwa kati ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran, ambayo yana kanuni kali na yamekuwepo kwa muda mrefu.
Amesema kinyume na ilivyo nchini Iran, nchi nyingi za Kiislamu zinazoandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani hazina vitabu maalum vya sheria kwa ajili ya mashindano hayo.
Katika mashindano ya Uturuki, wanapendelea maqari wanaoigiza wengine, alisema, na kuongeza kuwa wanataka qari wasishughulishwe na Lahn bali wazingatie usomaji mzuri, Sawt na sheria za Tajweed.
Akibainisha kwamba wataalamu wa Qur'ani kutoka nchi kumi walitathmini walisimamia mashindano hao, Angoshtan alisema kushinda taji katika hafla ya kimataifa ya Qur'ani sio kazi rahisi.
Alimshukuru Mwenyezi Mungu kwamba yeye na mwawakilishi wa Iran katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani nzima Milad Asheghi walifanikiwa kushika nafasi ya pili kila moja.
Wao, pamoja na washindi wengine, walitunukiwa katika hafla ya kufunga iliyofanyika Jumatano usiku, Oktoba 31, na kuhuhuduriwa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Asheghi pia alizungumza na IQNA alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini, akisifu mafanikio yake na ya Angoshtan kama wawakilishi wa Iran.
Aliwashukuru walimu wake wa Qur'ani, familia yake, hususan mama yake, na maafisa wa Qur'ani wa Iran kwa kuchangia katika mafanikio yake.
Amesema uzoefu wake katika mashindano yaliyopita na mashauriano na wahifadhi wa Iran waliohudhuria mashindano ya Qur'ani ya Uturuki katika miaka ya nyuma yalimsaidia kushinda daraja la pili.
Mashindano ya 9 ya kimataifa ya Qur'ani ya Uturuki yalifanyika kwa raundi mbili. Katika duru ya awali, iliyofanyika mwezi Juni, wawakilishi wa nchi 93 waliwasilisha video zilizorekodiwa za usomaji wao kwa kamati ya maandalizi. Baada ya tathmini ya faili na jopo la majaji, maqari na wahifadhi kutoka nchi 47 walifanikiwa kuingia fainali.
Mashindano hayo yalifanyika katika jiji la Sanliurfa kuanzia Oktoba 23-30.

captcha