IQNA

11:46 - May 28, 2019
News ID: 3471975
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Uturuki yamemalizika kwa kutunukwia zawadi washindi.

Sherehe za kufunga mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani zimefanyika Jumapili katika sherehe ambayo ilihudhuriwa na Rais Reccep Tayyib Erdogan wa Uturuki katika katika Msikiti wa Camlica mjini Istanbul.

Mashindano ya mwaka huu yalikuwa na washiriki 128 kutoka nchini 28 ambao walichuana kwa muda wa wiki moja.

Mshiriki kutoka Indonesia,  Syamsuri Firdaus ameshika nafasi ya kwanza katika kitengo cha Qiraa. Firdaus ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook na kumshukuru Allah SWT, wazazi, walimu, failia na marafiki kwa msaada wao katika mafanikio yake.

Mashindano hayo yamewaleta pamoja washiriki kutoka mabara ya Asia, Ulaya, Afrika na Amerika.

3468617

Name:
Email:
* Comment: