IQNA

20:21 - June 22, 2018
News ID: 3471568
TEHRAN (IQNA)-Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Jordan imetangaza mpango wa kuzindua vituo 50 vya kuhifadhi Qur'ani katika mkoa wa Karak nchini humo.

Heitham Bani Rashid, mkurugenzi wa wakfu katika wizara hiyo amesema vituo hivyo  vitawasaidia wanafunzi kutumia vizuri muda wao wa likizo za shule.

Amesema usajili wa washiriki wa kozi za Qur'ani Tukufu utaanza wiki ijayo na kwamba kati ya yatakayofunziwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani, misingi ya tajwedd n.k.

Aidha amesema kutakuwa pia na ratiba za masuala ya utamaduni katika Uislamu pembizoni mwa mafunzo hayo ya Qur'ani.

Ameongeza kuwa, kati ya vituo hivyo 50, 25 ni vya wavulana na vilivyosaliwa ni vya washichana na kuwamba kuna waalimu wa Qur'ani wenye uzoefu ambao watatoa mafunzo.

Halikadhalika amebaini kuwa kozi hizo za Qur'ani zinatolewa bila malipo na zitaendelea hadi mwisho wa mwezi wa Septemba.

 

3724262

Name:
Email:
* Comment: