IQNA

13:27 - November 18, 2018
Habari ID: 3471744

Kongamano kwa munasaba wa Maulid ya Mtume SAW nchini Tunisia

TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Masuala ya Kidini ya Tunisia imeandaa kongamano kuhusu Seerah ya Mtume Muhammad SAW.

Kongamano kwa munasaba wa Maulid ya Mtume SAW nchini Tunisia

Kongamano hilo la siku mbili lilikuwa la 46 na lilifanyika Jumamosi na Jumapili chini ya anuani ya "Seerah ya Mtume, Dhihirisho la Mfundisho ya Kiislamu na Thamani za Kijamii."

Kongamano hilo limefanyika katika mji wa Kairouna kaskazini mwa Tunisia kwa munasaba wa Maulid ya Bwana Mtume Muhammad SAW.

Wanazuoni na wasomi kutoka nchi kama vile Tunsia, Algeria, Morocco, Jordan, Kuwait, Saudi Arabia walihudhuria kongamano hilo.

3764804

captcha