IQNA

14:16 - January 08, 2019
News ID: 3471800
TEHRAN (IQNA)- Jamii nyingi za Waislamu nchini Marekani sasa zinakumbwa na tatizo la ukosefu wa Maimamu waliohitimu wenye uwezo wa kuongeza sala, kufanya kazi na vijana na kuongoza jamii ipasavyo.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Amerika Kaskazini, asilimia 44 tu ya Maimamu Marekani ndio wanaopata mshahara na wanaichukulia kazi hiyo kuwa kazi pekee kwa lengo la kuwahudumia Waislamu. Aghalabu ya  Maimamu ni wale waliojitolea kufanya kazi hiyo pasina kutegemea malipo.

Ronney Abaza, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kituo cha Kiislamu cha Noor katika mji wa Columbus, jimboni Ohio anasema wakati wakitafuta Imamu mwenye kutimiza masharti, walibaini kuwa wengi hawana uwezo wa kuhudumia jamii ya Waislamu.

Amesema kamati ya kumtafuta imami ilifanya kazi kwa muda wa miaka mitatu na hatimaye ilifanikiwa kumpata Sheikh Abdel Moneim kama kiongozi mpya wa jamii ya Waislamu katika eneo hilo Jumatano wiki iliyopita. Kabal ya kuchukua nafasi hiyo Sheikh Moneim alikuwa anahudumu katika mji wa Tampa jimboni Florida.

Ihsan Bagby, mhadhiri msaidizi wa Masomo ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Kentucky anaamini kuwa uhaba wa maimamu waliohitimu ni tatizo kubwa kwa jamii ya Waislamu Marekani.

Anabainisha zaidi kwa kusema kuwa tatizo si tu kupata Maimamu wenye uwezo bali ni ukosefu wa 'Imamu ambaye misikiti mingi inamhitaji, ni imamu ambaye ameinukia katika mazingira ya Marekani, mwenye elimu, anayeweza kufanya kazi na vijana Waislamu Marekani na pia mwenye uwezo wa kutoa mihadhara kwa wasiokuwa Waislamu na kushirikiana na viongozi wa dini zinginezo."

Anaongeza kuwa, kunai le nadharia kuwa Imamu ni mtu mwenye uwezo wa kuseoma Qur'ani na aliyehifadhi Qur'ani na mwenye ujuzi wa sheria za Kiislamu. Anasema Maimamu wanaohitajika ni wale weny uwezo wa kutoa ushauri nasaha na wanaoweza kuwa na uhusiano mzuri na vijana.

Takwimu zinaonyesha kuwa katika kila Maimamu watano Marekani, wanne walizalia na kuseoma nchi ya nchi hiyo ambapo aghalabu ni kutoka Misri, Saudi Arabia na India.

3467643

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: