IQNA

23:18 - April 17, 2019
News ID: 3471919
TEHRAN (IQNA)-Vijana Waislamu katika nchi 10 barani Ulaya wamewapa wapitanjia maua ya waridi na vijikaratasi vyenye maelezo ya kimsingi kuhusu Uislamu kwa lengo la kuondoa hofu na ubaguzi dhidi ya Uislamu na kustawisha maelewano katika jamii.

Harakati hiyo imeandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Milli Gorus  (ICMG) ina imezijumuisha nchi za Ujerumani, Uholanzi, Austria, Ubelgiji, Ufaransa, Denmark, Norway, Sweden, Italia na Uswisi. Huu ni mwaka wa siku wa kufanyika harakati hiyo ya kila mwaka yenye anuani ya  "Hujambo, Mimi ni Mwislamu."

Milli Gorus ni taasisi yenye miziz ya Uturuki na wanaoshiriki katika harakati hiyo ni Waislamu wenye asili mbali mbali.

Jumuiya ya Kiislamu ya Milli Gorus  (ICMG) ilifungua ofisi yake Ujerumani muongo wa sabini na sasa ina wanachama karibu 87,000 kote Ulaya ambao hutoa mchango wa mamilioni ya Euro kwa ajili ya kufadhili harakati za Kiislamu.

ICMG ina misikiti na vituo vya utamaduni 514 katika nchi 11 za Ulaya. Kampeni ya "Hujambo, Mimi ni Mwislamu" inafanyika huku kukiwa na wimbi kubwa za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika nchi za Magharibi. Moja ya sababu kuu za hali hiyo ni kukosekana maelezo ya msingi kuhusu Uislamu.

3468324/

Name:
Email:
* Comment: