IQNA

12:35 - May 11, 2019
News ID: 3471951
TEHRAN (IQNA)-Zaidi ya wafungwa zaidi ya 100 Wahindu wamejiunga na wafungwa Waislamu katika Sawm ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mjini New Delhi, India.

Katika taarifa, Gereza ya Tihar imesema kati ya wafungwa 16,664 katika magereza 16 mjini New Delhi, 2,658 wanashiriki katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Taarifa hiyo imesema wafungwa 110 Wahindu wamejiunga na Waislamu katika Sawm ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Taarifa hiyo imesema wakuu wa magereza wameweka ratiba maalumu ya chakula ili kuhakikisha kuwa wafungwa wanapata futari na daku kwa wakati.

Aidha wafungwa walio katika Sawm pia  wanapewa fursa zaida ya kuswali katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 

Halikadhalika mashirika ya kidini yanaruhusiwa kuwatembelea wafungwa kwa ajili ya kuwapa futari na kushiriki nao katika Sala. Mji wa New Delhi una magereza matatu ambayo ni Tihar, Rohini na Mandoli.

3810413

Wafungwa Wahindu wajiumuika na Waislamu katika Sawm ya Ramadhani New Delhi

Name:
Email:
* Comment: