IQNA

23:37 - June 27, 2019
News ID: 3472019
TEHRAN (IQNA)- Aghalabu ya Wapalestina wanapinga vikali mpango wa Muamala wa Karne na kikao cha uchumi kulichofanyika hivi karibuni mjini Manama, Bahrain.

Kictuo cha Uchunguzi wa Fikra na Maoni katika Chuo Kikuu cha al-Aqsa cha Ukanda wa Ghaza, Palestina kimetangaza kwamba matokeo ya uchunguzi uliofanywa katika eneo hilo, unaonyesha kwamba asilimia 98.4 ya Wapalestina wanaoishi eneo la Ukanda wa Ghaza, wanapinga vikali mpango wa Muamala wa Karne na kikao cha uchumi kulichofanyika hivi karibuni mjini Manama, Bahrain.

Uchunguzi uliofanyika kati ya tarehe 18 hadi 23 ya mwezi huu umeonyesha kwamba asilimia 99.3 ya watu walioulizwa kuhusiana na suala hilo walisema kwamba, kuendelea mpasuko ndani ya Palestina ndiko kumeishajiisha serikali ya Marekani kuandaa mpango huo wa Muamala wa Karne. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, asilimia 97.6 ya watu waliotoa majibu yao walisema kwamba lengo la Muamala wa Karne ni kuisambaratisha kabisa Palestina na kufumbia macho haki za Wapalestina na kuongeza kuwa hali ya sasa ya kieneo na kimataifa huenda ikasaidia mpango huo. Kadhalika asilimia 99.1 ya washiriki wa uchunguzi huo wa maoni sambamba na kupongeza msimamo wa Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO kwa hatua yake ya kupinga Muamala wa Karne, wanaamini kwamba upinzani uliopo utapelekea kusambaratika kwa mpango huo wa Marekani.

Uchunguzi umeendelea kubainisha kwamba, asilimia 98.9 ya walioshiriki wamesisitiza kuwa, kikao cha kiuchumi cha mjini Bahrain, ilikuwa njama ya kuwashawishi Wapalestina wakubali mpango huo na kwamba kushiriki kikao hicho. Kikao cha siku mbili ambacho ni hatua ya awali kwa ajili ya kutekelezwa mpango wa Muamala wa Karne, kilianza siku ya Jumanne mjini Manama, Bahrain. Kwa mujibu wa mpango huo mjii wa Quds utakabidhiwa utawala wa Kizayuni huku badala yake mji wa Abu Dis ukiwa ndio utakaofanywa mji mkuu wa Palestina, wakimbizi wa Kipalestina wanaoishi katika nchi mbalimbali hawatakuwa na haki ya kurejea katika ardhi zao asilia na Wapalestina watabakia na ardhi iliyosalia katika eneo la Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, suala ambalo limepingwa ndani na nje ya Palestina.

Kikao cha siku mbili cha mpango wa 'Muamala wa Karne' kilimalizika jana Jumatano huko Manama, mji mkuu wa Bahrain huku kukiwa na maandamanao na malalamiko makubwa ya raia wa nchi za Asia Magharibi dhidi yake.

Kikao hicho kinadaiwa kufanyika kwa lengo la kuvutia uwekezaji wa kigeni kwa maslahi ya Wapalestina. Marekani ambayo imeandaa na kusimamia kikao hicho, inafanya njama za kutumia ibara za hadaa za kiuchumi na uwekezaji kwa ajili ya kupunguza makali ya malalamiko na upinzani wa Wapalestina dhidi ya mpango huo.

Bila shaka kikao cha Manama kimefanyika kwa madhumuni ya kulinda maslahi ya utawala haramu na kibaguzi wa Israel. Baadhi ya habari za siri zilizofichuka hivi karibuni zinasema kuwa utawala ghasibu wa Israel uliwakilishwa katika kikao hicho na ujumbe wa siri ambao uliketi pembeni ya baadhi ya nchi saliti za Kiarabu. Mbali na hayo baadhi ya ripoti zinasema kwamba waandishi wa magazeti na wapiga picha 20 wa vyombo vya habari vya Israel walishiriki kikao hicho.

/3468850

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: