IQNA

Makamanda wawili wa harakati ya Jihad Islamu ya Palestina wauawa shahidi katika hujuma ya Israel

20:16 - November 13, 2019
Habari ID: 3472213
TEHRAN (IQNA)- Makamanda wawili wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina wameuawa aktika hujuma mpya za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Brigedi za Quds, Tawi la Kijeshi la Jihad Islami, Baha Abu al-Ata, kamanda wa Kikosi cha al-Quds aliyekuwa na umri wa miaka 42, aliuawa shahidi katika shambulizi la anga la jeshi la Israel dhidi ya makazi yake katika Ukanda wa Gaza mapema  Jumanne.

Muda mfupi baada ya mauaji hayo, wanamuqawama wa Palestina wameanzisha mashambulizi ya ulipizaji kisasa kwa kuvurumisha maroketi dhidi ya Israel, ambayo yamelenga miji ya Tel Aviv, Sderot na Ashdod.

Utawala haramu wa Israel umetiwa kiwewe na mashambulizi hayo ya ulipizaji kisasi, na umewataka wanafunzi na wanachuo wasiripoti shuleni na vyuoni katika mji mkuu Tel Aviv na miji mingine mikubwa, sawa na wafanyakazi 'wasio wa dharura'.

Kufuatia kuendelea hujuma hizo za utawala wa Kizayuni wa Israel, kamanda mwingine wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina ameuawa shahidi katika hujuma ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Khalid Mavaz Faraj ambaye alikuwa kamanda wa wapiganaji wa harakati hiyo kati mwa Ghaza ameuawa shahidi katika shambulizi la anga la jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimetangaza kuwa, kufuatia kuvurumishwa makombora ya makundi ya wanamuqawama na wapigania ukombozi wa Palestina ambayo yamelenga ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, watu 41 wamejeruhiwa.

Tokea mwaka 2006, utawala wa Kizayuni wa Israel uliweka mzingiro wa nchi kavu, anga na baharini dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza. Katika mzingiro huo, Israel inazuia bidhaa muhimu kama vile, petroli, umeme, dawa, chakula na vifaa vya ujenzi kufika katika Ukanda wa Ghaza.

Wanamuqawama na wapigania ukombozi wa Palestina wameapa kuendeleza harakati zao hadi pale ardhi zote za Palestina zitakapokombolewa kutoka katika makucha ya utawala dhalimu wa Israel.

3469864/

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :