IQNA

18:00 - September 22, 2019
News ID: 3472143
TEHRAN (IQNA) -Magaidi kundi la al-Shabab wamedau kuua wanajeshi 23 wa Somalia katika hujuma dhidi ya kituo kimoja cha jeshi.

Afisa mmoja wa Somalia ameziambia duru za habari mjini Mogadishu kwamba, watu waliokuwa na silaha wanaosadikiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la al Shabab wamefanya shambulio dhidi ya kambi moja ya jeshi mjini humo. Shambulizi hilo limejiri Jumapili asubuhi nje kidogo ya mji wa bandairni wa Marka, mji mkuu wa jimbo la Lower Shabelle, yapata kilomita 100 kusini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Duru za usalama zinadokeza kuwa raia 13 wameuawa katika shambulizi hilo huku makumi ya wengine wakijeruhiwa.

Msemaji wa kundi la kigaidi la al Shabab Abdiasis Abu Musab amesema wametekeleza shambulizi hilo kwa kutumia gari lililokuwa limesheni mabomu na kwamba baada ya gari hilo kulipuka wapiganji wa kundi hilo walianza kufyatua risasi kiholela.  Aidha amedai kuwa wapiganaji wa Al Shabab wamepora magari ya dera ya Jeshi la Somalia katika shambulio hilo.

Shambulio hilo linatokea siku tatu tu baada ya watu wengine watatu kupoteza maisha yao katika shambulizi la bomu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, shambulio ambalo nalo lilitekelezwa na wanamgambo wa al-Shabab.

Kundi la kigaidi la al Shabab lilianza hujuma zake nchini Somalia mwaka 2007 na limekuwa likiendesha ugaidi katika mji mkuu Mogadishu na maeneo mengine ya Somalia na pia katika nchi jirani ya Kenya. Magaidi hao walitumuliwa Mogadishu Agosti 2011 katika operesheni iliyofanywa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika AMISOM, lakini limekuwa likifanya mashamabulizi ya kuvizia mara kwa mara.

AMISOM ina askari wapatao 21,000 nchini Somalia ambao wanalinda amani katika nchi hiyo inayosumbuliwa na vita vya ndani kwa robo karne sasa.

Kundi la kigaidi la al Shabab, sawa na Boko Haram, Al Qaeda, ISIS ,  lina ufahamu usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa likitekeleza hujuma katika maeneo mbalimbali ya Somalia na nchini Kenya.

3469468

Name:
Email:
* Comment: