IQNA

18:46 - November 01, 2019
News ID: 3472196
TEHRAN (IQNA) – Raia zaidi ya 100,000 wameuawa nchini Yemen tokea Machi 2015 wakati Saudi Arabia ilipoanzisha vita dhidi ya Yemen.

Kwa mujibu wa  asasi inayojulikana kama Mradi wa Maeneo ya Vita na Data (ACLED) wenye makao yake Marekani, vita hivyo vinavyoongozwa na  Saudia dhidi ya Yemen  idadi hiyo inajumuisha pia zaidi raia 12,000 ambao wameuawa moja kwa moja katika vita.

Ripoti hiyo imebaini kuwa watu 20,000 wameuawa katika vita mwaka huu na kuufanya kuwa wa pili kwa idadi ya watu walipoteza maisha kutokana na vita baada ya mwaka 2018.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha usukani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh.

Hata hivyo Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao hayo huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasio na hatia. Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia kwa himaya ya madola ya Magharibi hasa Marekani na utawala haramu wa Israel.

3469775

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: