IQNA

Binti Muislamu aliyevaa Hijabu ni Mwanamichezo Bora Msichana Uingereza

6:10 - November 24, 2019
Habari ID: 3472228
TEHRAN (IQNA) –Binti Muislamu mwenye kuvaa Hijabu, Khadijah Mellah, ametangazwa kuwa Mwanamichezo Bora Msichana wa mwaka nchini Uingereza kufuatia ushindi wake katika mashindano ya mbio za farasi ya Kombe la Magnolia.

Mellah, alikuwa mshiriki wa kwanza wa kike kushiriki katika mashindano rasmi ya farasi nchini Uingereza akiwa amevalia Hijabu na aligonga vichwa vya habari baada ya kufanikiwa kuendesha farasi Haverland hadi kupata ushindi katika mashindano yaliyofanyika Goodwood mwezi Agosti.

Mellah amekabidhiwa zawadi yake katika ofisi cha News UK mjini London katika sherehe iliyofanyika Alhamisi.  Khadijah Mellah aliye na umri wa miaka 18 anasema anafuraha kubwa kuwa ameweza kutoa taswira chanya ya mwanamke Muislamu mwenye kuvaa Hijabu nchini Uingereza. Aidha amesema kumekuwepo na taswira potovu nchini humo kuhusu wanawake Waislamu kuwa hawatoki nje ya nyumba na kufanya kazi za kawaida.  Novemba 2 Televisheni ya ITV ilirusha hewani filamu ya matukio ya kweli iliyopewa jina la 'Riding Dream' kuhusu namna ambavyo Mellah alianza kuendesha farasi hadi kupata ushindi. 

Mellah ni binti mnyenyekevu na anaendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Brighton. Bi. Khadijah Mellah, ambaye mama yake ni Mkenya na baba yake ni Mualgeria, anasema amepokelezwa vizuri na wenzake katika mashindano ya farasi.

Binti Muislamu aliyevaa Hijabu ni Mwanamichezo Bora Msichana Uingereza

Bi. Khadijah Mellah akiwa na wazazi wake

 

Binti Muislamu aliyevaa Hijabu ni Mwanamichezo Bora Msichana Uingereza

3858805

captcha